Mwili wa Mugabe wapelekwa kijijini kwake


0

Mwili wa rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe unatarajiwa kupelekwa  kijijini kwake leo kwa ajili ya mkesha wakati maziko yake yakiandaliwa katika muda wa karibu mwezi mmoja.

Mugabe alifariki dunia wiki moja iliyopita akiwa na umri wa miaka 95 nchini Singapore, alipokuwa akitibiwa ikiwa ni takribani miaka miwili tangu alipoondolewa madarakani kwa nguvu ya Jeshi mnamo mwaka 2017.

Baada ya msiba wa kitaifa jana Jumapili katika mji mkuu Harare ambapo ulihudhuriwa na viongozi kadhaa wa mataifa ya Afrika, akiwemo Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa na Rais wa Kenya Uhuru Kenyata.

Mwili wake utapelekwa kijijini kwake Katama, umbali wa karibu kilomita 90 kuelekea magharibi mwa Zimbabwe, kuwaruhusu wanakijiji kutoa heshima zao za mwisho na kumuaga. Mpwa wake Leo Mugabe amesema mwili wa Mugabe utalala kijijini hapo usiku wa leo na kurejeshwa mjini Harare kesho Jumanne kwa ajili ya kihifadhiwa.

Taratibu za mazishi ya mwisho ya Mugabe zilikumbwa na mgogoro kati ya Rais Emmerson Mnangagwa na familia yake, kuhusiana ma mahali kiongozi huyo wa zamani anapopaswa kuzikwa.

 


Like it? Share with your friends!

0