Mwili wa Mugabe kuzikwa Jumamosi


0

Wanafamilia wa aliyekuwa Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe pamoja na maafisa wa serikali wameelekea nchini Singapore kuuchukua mwili wa kinara huyo wa siasa za Afrika aliyefariki dunia wiki iliyopita.

Mpwa wa Mugabe, Leo Mugabe amesema ndege inayokwenda kuuchukua mwili wa Mugabe imeondoka jijini Harare leo asubuhi na inatarajiwa kurudi nchini humo keshokutwa.

 Kwa mujibu wa taaarifa iliyochapishwa na Idhaa ya Kiswahili ya DW, utakapowasili nchini humo, mwili huo utachukuliwa moja kwa moja kupelekwa kijijini kwake huko Zvimba, kama kilomita 90 magharibi mwa Harare kwa ajili ya mkesha kabla ya maziko.

 Alhamisi na Ijumaa, mwili huo utawekwa katika uwanja wa Rufaro kitongoji cha Mbare jijini Harare ili wananchi waweze kumuaga kwa mara ya mwisho.

 

Mugabe alifariki akiwa nchini Singapore alipokuwa akitibiwa kwa muda mrefu na amefariki akiwa na umri wa miaka 95.


Like it? Share with your friends!

0