Mwanaharakati Mmusi Maimane ataka haki kwa Zitto Kabwe


0

AFRIKA KUSINI

Mwanaharakati na mwanzilishi wa taasisi ya One South Africa Movement (OSA) ya nchini Afrika Kusini, Mmusi Aloysias Maimane ametoa wito wa kuachiwa kwa kiongozi wa chama cha upinzani nchini ACT Wazalendo, Zitto Kabwe baada ya kukamatwa na askari polisi akiwa katika mkutano wa ndani wa wanachama.


Siku ya jana Zitto Kabwe na wanachama wengine takribani nane walikamatwa na polisi kwa madai kuhamasisha na kufanya mkusanyiko batili.

Picha video ya kukamatwa kwa kiongozi huyo na wenzie ilitawala katika mitandao ya kijamii muda mfupi baada tukio hilo na baadae chama hicho kilithibisha kukamnatwa kwake.

Kufuatia tukio hilo wanaharakati mbalimbali wamekuwa wakipaza sauti zao katika mitandao ya kijamii wakishinikiza kuachiliwa kwa kiongozi huyo.

Mmusi Aloysias Maimane mwanaharakati mashuhuli Afrika ya Kusini  ametuma taarifa kwa waandishi pamoja na ujumbe wa video akitoa wito kwa Umoja wa Afrika kupitia rais wa Afrika kusini Cyril Ramaphosa ambaye ni mwenyekiti wa Umoja huo kuingilia kati suala hilo ili kulinda haki ya demokrasia nchini.

Maimane ambaye pia aliwahi kuwa kiongozi wa chama cha upinzania cha Democratic Alliance cha Africa Kusini amesema wataandikia ujumbe kwa Ramaphosa ili kwa uwezo wake ahakikishe sheria inachukua mkondo wake na Zitto kabwe analindwa na anapata haki anayostahili.

Anaeleza kuwa Zitto Kabwe ni kiongozi wa chama cha upinzani na anajiandaa na uchaguzi wa October 2020 lakini wamemkamata akiwa katika mkutanno wa ndani suala ambalo halikubaliki.

Zitto Kabwe na viongozi wenzake walisafirishwa jana usiku kwa gari la wazi kutoka Kilwa hadi Lindi na Mawakili wa chama hicho wapo mkoani humo na wanashughulikia Dhamana.

Mkuu wa jeshi la polisi mkoani Lindi Stanley Kulyamo amesema jeshi la polisi mkoani humo lililazimika kuwakamata Viongozi wa chama cha ACT Wazalendo kwa sababu walifanya maandamano bila kuwa na kibali.

Kwa mujibu wa kituo cha redio cha Mashuja cha mkoani Lindi RPC Kulyamo amesema walipata taarifa za siri juu ya mchakato wa kikao cha ndani wa chama hicho lakini walishangaa kuona watu wakiandamana bila taarifa.


Like it? Share with your friends!

0