Museveni afikiria kuahirisha uchaguzi mkuu


0

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema ni wendawazimu kwa nchi kufanya uchaguzi wakati huu wa mlipuko wa virusi vya corona.

Museven ameliambia shirika la habari la Uganda (NBS), kwamba mipango ya kufanya uchaguzi mapema mwaka 2021 haitakuwepo kama virusi vya corona havitadhibitiwa, na itatakiwa kuangaliwa upya.

Museven ametoa kauli hiyo wakati takribani wagombea 24 nchini humo wametangaza ni ya kuwania urais, na wameshawasilisha maombi yao kwa Tume ya Uchaguzi Uganda ili kumkabili Rais Museveni aliyepo madarakani tangu mwaka 1986.

Hata hivyo mikutano ya wazi ikiwemo ya kisiasa imepigwa marufuku kama sehemu ya hatua za kutosogeleana na watu wametakiwa kukaa nyumbani kwa ajili ya kuzuia kusambaa kwa virusi vya corona.

Kauli ya Museveni imeibua mijadala na maswali mengi kwa raia nchini humo na ikiwemo ni je kweli uchaguzi nchini Uganda hautakuwepo au lah. Uganda ina jumla ya visa 122 vya maambukizi ya virusi vya Corona


Like it? Share with your friends!

0