Mtifuano Ndugai na Bulaya


0

Ikiwa ni siku moja imepita tangu Spika wa Bunge Job Ndugai kutoa mashart mawili kwa wabunge wa Chadema waliojitenga kwa siku 14 na kutohudhuria vikao vya bunge, kuwataka kuwasilisha ushahidi kwamba wamepimwa na hawana maambukizi ya virusi vya corona kabla ya kuruhusiwa kuingia bungeni, leo wabunge hao 15 wamepanga kurejea bungeni. Je, wametimiza mashart waliyopewa na Spika Ndugai? Kwanza TV imeongea na Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni ambaye pia ni mbunge wa Bunda, Ester Bulaya anaelezea kwa njia ya simu.

 


Like it? Share with your friends!

0