Mnyika kwa Spika Ndugai ‘Maamuzi yako yanachafua Bunge’


-1
-1 points

Kambi ya Upinzani Bungeni, imemtaka Spika wa Bunge, Job Ndugai, kutengua uamuzi wake wa kusimamisha vikao vya kamati za Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), na Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa(LAAC).

Mwakilishi wa Kambi ya Upinzani, John Mnyika amesema maamuzi aliyoyatoa Spika hayana tija kwa kuwa yanahusianisha mgogoro baina yake na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Prof.Musa Assad, na hivyo amemtaka kubadilisha uamuzi wake na kamati hizo ziweze kukutana kabla ya tarehe 25 Januari, na licha ya hivyo Bunge bado lina wajibu wa kupokea taarifa za mwaka kuanzia Januari 2018/2019 kwa kamati zote.

Kadhalika Mnyika ameongeza kuwa kitendo kilichoonyeshwa na Spika Ndugai cha kutangaza kutoshirikiana na CAG, ni jambo lisilokubalika, kwa kuwa ni kinyume cha sheria na kanuni za Bunge, lakini pia linaweka taswira mbaya kwa mhimili huo.


Like it? Share with your friends!

-1
-1 points