Mke wa Rais Nkurunziza apelekwa Kenya kutibiwa Corona


2
2 points

Nairobi, Kenya

Mke wa rais wa Burundi, Denise Bucumi Nkurunziza amelazwa katika hospitali ya chuo kikuu cha Aga Khan jijini Nairobi baada ya kuripotiwa kuwa na maambukizi ya virus vya corona.
Vyanzo vya habari vinasema Denise Bucumi alipelekwa Kenya na ndege ya wagonjwa kutoka shirika la AMREEF la nchini Kenya siku ya Alhamisi akisindikizwa na walinzi watatu, ambapo mmoja wao pia amekutwa na maambukizi ya virusi hivyo.
Vyanzo hivyo vinaongeza kuwa kabla ya Denise kuwasili uwanjani hapo wafanyakazi wa uwanja wa ndege na polisi waliondolewa kwa muda wa takribani dakika 20. Wanasema aliwasili uwanja wa ndege wa Bujumbura na msafara wa gari tano ikiwemo gari ya jeshi iliyokuwa inampa ulinzi na hakufuata taratibu za kujisaili kama ilivyo kawaida.
Mume wa Denise, Pierre Nkurunziza hakuwepo kwenye ndege hiyo na mpaka sasa hakuna taarifa zozote juu ya maendeleo ya afya yake.
Haijawekwa wazi ni kwa namna gani ameingia Kenya wakati huu ambao nchini hiyo imeweka masharti ya kuruhusu wasio na maambukizi ya virusi vya corona pekee kuingia katika nchi hiyo.

Rais Nkurunziza amekuwa akikosolewa kwa namna anavyoshughulikia janga la virusi vya corona nchini kwake.
Burundi ndio nchi pekee barani Afrika ambayo haikusimamisha michezo ya mpira wa miguu ili kuzuia kuenea mwa maambukizi ya virusi vya corona.

Nchi hiyo pia imefanya uchaguzi mkuu wa Urais hivi karibuni na mgombea wa chama tawala Evariste Ndayishimiye aliibuka mshindi kwa asilimia 69 ya kura zote.
Siku ya Alhamisi wakati wa maombi ya kitaifa ya kumshukuru Mungu kwa ushindi wa chama tawala katika uchaguzi huo, Nkurunziza alisema kuwa mkono wa Mungu umewaokoa na janga la corona.
Majuma mawali yaliyopita Burundi iliwaamuru wawakilishi wa Shirika la Afya Duniani WHO na wataalam wengine wa afya waliokuwa wakishughulikia mlipuko wa virusi vya corona kuondoka nchini humo.

 


Like it? Share with your friends!

2
2 points