Milioni 15.2 za vitambulisho vya Magufuli hazijulikani zilipo


0

Katibu tawala Wilaya ya Mbozi, Tusubilege Benjamin amesema Sh15.2milioni za mauzo ya vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo 760  katika halmashauri ya Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe, hazijulikani zilipo.

Mkuu huyo wa Wialaya ameyasema hayo katika kikao cha watendaji wa vijiji, kata, wakuu wa idara za halmashauri na madiwani.

Amesema Wilaya ya Mbozi ilikabidhiwa vitambulisho 15,480, na waliopewa kwa ajili ya kuwapatia wafanyabiashara wadogo ni watendaji na baadhi yao wameshindwa kuwasilisha fedha ama vitambulisho hivyo.

Benjamin amewaonya watendaji walioshindwa  kuwasilisha vitambulisho hivyo ama fedha kuwa wanahatarisha ajira yao.

Mara ya kwanza Rais Magufuli alitoa vitambulisho 670,000 kuwatambua wafanyabiashara wadogo nchini Tanzania, kuhakikisha wanafanya shughuli zao bila kusumbuliwa, ambapo alisema kwa muda mrefu amekuwa akiiagiza TRA pamoja na halmashauri kutowatoza kodi wajasiriamali wadogo ambao mitaji yao haizidi Sh4 milioni, lakini utekelezaji wake umekuwa wa kusuasua.

Kila Mkoa ulipewa vitambulisho 25,000, na kila mjasiriamali mdogo alilipia Sh20,000 na fedha hiyo kupelekwa TRA. Kwa malipo hayo, kila mkuu wa mkoa alipaswa kukusanya Sh500 milioni na ikilazimu aagize vitambulisho vingine kwa ajili ya watakaovihitaji.


Like it? Share with your friends!

0