Mfahamu mhubiri aliyetabiri kifo cha Rais Nkurunzinza mwaka mmoja uliopita


2
2 points

Makamba, Burundi

Mhubiri aliyejulikana kama Nabii Pierre Barakikana wa kanisa la kievanjelisti la Emmanuel alikamatwa na kufungwa gerezani tarehe 8 mwezi wa sita mwaka 2019. Kama mkazi wa wilaya ya Bubanza, kijiji cha Mpanda, Barakakina alishtakiwa wilaya ya Makamba baada ya kukamatwa na polisi tarehe 29 mwezi wa tano mwaka jana .

Kwa mujibu wa shirika la utetezi wa haki za binadamu nchini Burundi, SOS Burundi, mashahidi walieleza kuwa “Nabii” Barakikana alipita mitaani akihubiri kuwa pigo la ugonjwa litaikumba Burundi na Rais Nkurunziza atafariki. Jambo hili lilimfadhaisha sana gavana wa Makamba, Gad Niyukuri aliyeagiza akamatwe mhubiri huyu na akahamishwa gereza la Murembwe, huko Makamba

Pierre Barakikana akiwa gerezani aliendelea kusisitiza kuwa unabii aliyoupata ulikuwa wa kweli. Kwa mujibu wa mtandao wa habari wa Burundi Daily, ‘nabii’ Barakikana alisisitiza kuwa ni msemaji wa Roho Mtakatifu na yuko tayari kufa kuliko kunyamzishwa. 

Tarehe 8 mwezi wa sita mwaka huu, mwaka mmoja baadaye, Rais Nkurunzinza alifariki dunia. Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC na vyanzo vingine ndani ya Burundi, rais huyu alifariki kwa ugonjwa wa Corona ambao umekuwa ukiikumbuka dunia nzima.  Hata hivyo taarifa rasmi ya serikali ya Burundi ilieleza kuwa alifariki kwa mshtuko wa moyo akiwa na umri wa miaka 55. Mke wake Rais alipelekwa nchini Kenya kwa  ajili ya matibabu ya ugonjwa wa Corona kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Kenya.

Rais Nkurunzinza ambaye alikuwa amemaliza muda wake, alipanga kumkabidhi madaraka rais mteule Evariste Ndayishimiye mwezi wa nane. Rais Nkurunzinza alikataa kufuata mwongozo wa Shirika la Afya Duniani (WHO) kuhusu njia za kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona na aliwafukuza wawakilishi wa shirika hilo nchini.


Like it? Share with your friends!

2
2 points