Mbowe anyang’anywa Ofisi jimboni


0

Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya, amemnyang’anya ofisi ya ubunge mbunge wa jimbo hilo, Freemani Mbowe na kuwapa Idara ya Uhamiaji, baada ya kuona ofisi hiyo imefungwa wakati wote, hali ya kuwa kuna idara za umma hazina sehemu ya kufanyia shughuli zao.

Sabaya amesema kuwa Mbowe hajaitumia ofisi hiyo tangu mwaka 2010 na tangu achaguliwe, pia hajawahi kuingia katika ofisi hiyo kusikiliza kero za wananchi wakati wanancho hao wanahitaji huduma.

Ameongeza kuwa lengo la Serikali kutoa ofisi kwa mbunge huyo, ilikuwa ni kuwasaidia wananchi kufika hapo na kutatuliwa shida zao, lakini cha kushangaza haikuwa inafunguliwa n ahata alipochungulia ndani ya ofisi hiyo alikua uchafu ulioambatana na buibui, tandu na wadudu wengine.

MWISHO


Like it? Share with your friends!

0