Mayweather kugharamia mazishi ya Floyd


-1
-1 points

Houston,Marekani

Bingwa wa ndondi, Floyd Mayweather amejitolea kulipa gharama za mazishi ya George Floyd, Mmarekani mweusi aliyefariki wiki iliyopita akiwa mikononi mwa polisi wa jimbo la Minneapolis nchini Marekani.
Kifo cha Floyd kilizua gumzo baada ya video iliyokuwa ikisambaa zaidi kupitia mitandao ya kijamii, ikimuonyesha afisa wa polisi, Derek Chauvin akimkandamiza kwa mguu eneo la shingoni (Floyd), huku maafisa wengine wawili wakimzuia.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mayweather Promotions, Leonard Ellerbe alithibitisha kuhusika kwa bondia huyo kulipia gharama za mazishi hayo.

Mazishi ya Floyd yanatarajiwa kufanyika katika mji wake wa Houston, Juni 9, mwaka huu.
Wakati hayo yakijiri, uchunguzi wa kimatatibabu umeonyesha kuwa Floyd alifariki kwa kukosa hewa ya oksijeni, kulikotokana na kukandamizwa shingoni.
Pia uchunguzi huo ulibaini kuwa matatizo ya afya yalichangia kwa kiasi kikubwa kutokea kifo cha Floyd.
Tukio hilo limesababisha maandamano ya siku sita mfululizo kote Marekani na machafuko ambayo hayajawahi kushuhudiwa kwa miongo kadhaa katika maeneo mbalimbali nchini humo.

 

 

 


Like it? Share with your friends!

-1
-1 points