Masikini Zitto Kabwe!


1
1 point

Lindi, Tanzania

Wanadaiwa kuwa ni askari polisi wakivamia mkutano wa ndani wa wanachama wa chama cha ACT- Wazalendo, uliotarajiwa kufanyika leo katika wilaya ya Kilwa mkoani Lindi.

Kuna video imesambaa kupitia mitandao ya kijamii muda mfupi kabla ya mkutano huo kuanza. Wanachama wa chama hicho waliohudhuria mkutano huo wanaonekana kushangazwa na kitendo hicho hasa pale polisi walipoondoka na Kiongozi Mkuu wa0, Zitto Kabwe. Inadaiwa kwamba hakuna maelezo yoyote yaliyotolewa kuhusu sababu za kumkamata mwanasiasa huyo.

Kabwe amekamatwa mapema asubuhi ya leo kabla ya kuanza mkutano huo wa ndani. Pia walikamatwa wanachama wengine akiwemo aliyekuwa Mbunge wa Kilwa Kusini, Selemani Bungara maarufu kama ‘Bwege’ na Sheweji Mketo ambaye ni Katibu Kamati ya Oganaizesheni ya chama hicho.

Baadhi ya wanachama wanailalamikia dola kwa kuwanyanyasa wapinzani.

Hata hivyo taarifa iliyotolewa na chama hicho muda mchache baadae imeeleza kuwa, mara baada ya viongozi hao kufikishwa polisi walihojiwa juu ya tuhuma za kuhamasisha na kufanya mkusanyiko batili.

Kumekuwa na mfululizo wa matukio ya kukamatwa na kuwekwa rumande viongozi wa upinzani, jambo ambalo limekuwa likilalamikiwa kuwa linavunja misingi ya demokrasia uhuru wa kujieleza.


Like it? Share with your friends!

1
1 point