Marekani yainyooshea kidole Tanzania


-1
-1 points

TANZANIA

Marekani imeibuka kwa mara nyingine tena ikielezea kusikitishwa kwake na kile ilichokiita kuminywa kwa misingi ya demokrasia nchini.
Hayo yamo kwenye tamko la ubalozi wa nchi hiyo leo, likigusia vitendo vya kukamatwa viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani wakiwa katika vikao vyao vya ndani na kufuta leseni ya gazeti la Tanzania daima.
Ubalozi huo umeeleza kuwa hatua hizo ni mwendelezo wa mlolongo wa matukio ya kusikitisha na ya vitisho kwa wapinzani, asasi za kiraia na vyombo vya habari.

Taarifa hiyo pia imesema haki ya kukusanyika kwa amani na uhuru wa kujieleza ni mambo yaliyojumuishwa na yanayolindwa na Katiba ya Tanzania na tamko la kimataifa la haki za binadamu.
Hata hivyo, ubalozi huo umesema una fahari ( hapa ni una fahari ama upo tayari?) kusaidia na kuunga mkono uhuru wa kujieleza na ushiriki jumuishi wa kisiasa kwa namna zote.
Tamko hilo limetoka ikiwa tayari katika muda wa wiki hii, matukio matatu ya namna kama yaliyotajwa katika tamko la ubalozi huo yametokea ikiwamo kufutiwa leseni kwa gazeti hilo, kukamatwa kwa viongozi wa chama cha ACT – Wazalendo na pia wafanyakazi wa kituo cha Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC).

 

 

 

 


Like it? Share with your friends!

-1
-1 points