Marekani yafuta mazungumzo na Taliban


0

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Mike Pompeo amesema kundi la Taliban lilivuka mipaka kwa kufanya shambulio la bomu lililotegwa ndani ya gari, karibu na ubalozi wa Marekani mjini Kabul.

Shambulio hilo lilosababisha kifo cha mwanajeshi mmoja wa Marekani, limesababisha Donald Trump kufuta mazungumzo ya amani na kundi hilo, yaliyopangwa kufanyika Camp David.

Pompeo amesema sasa ni juu ya Taliban kubadilisha mwenendo wao. Mwanadiplomasia huyo hakutaja mazungumzo hayo ya amani yatapangwa lini kufanyika tena.

Wakati huo huo raia wa Afghanistan wanajiandaa na uwezekano wa kutokea ghasia kutoka Taliban baada ya Trump kuyafuta kwa ghafla mazungumzo na kundi hilo la wanamgambo, ambalo limeapa kuendeleza vita dhidi ya kile linachokiita uvamizi wa kigeni.


Like it? Share with your friends!

0