Marekani na Uingereza zanyooshea kidole Tanzania kwa kukiuka haki ya kisheria


0

Marekani na Uingereza zimeelezea wasiwasi wao juu ya utawala wa sheria unavyozidi kuporomoka nchini Tanzania na kutaja juu ya kukamatwa kwa Erick Kabendera.

Katika taarifa yao ya pamoja mataifa hayo yamesema yanawasiwasi jinsi mwandishi huyo alivyokamatwa, kuzuiliwa na kushitakiwa pamoja na kunyimwa haki ya kuwa na wakili, wakati alipokamatwa ambapo ni kinyume na utaratibu wa sheria ya makosa ya jinai.

Kabendera, anayefahamika kwa kuandika taarifa za kuikosoa Serikali ya Rais John Magufuli, alishtakiwa wiki hii kwa makosa ya kupanga uhalifu, kukwepa kodi na utakatishaji wa fedha baada ya kukamatwa nyumbani kwake na Polisi waliyovalia kiraia mnamo Julai 29.

Kukamatwa kwake kumezua hisia tofauti miongoni mwa watetezi wa haki za binaadamu, waliotaka Kabendera kuachiwa huru, na kuonya kesi hiyo inaonyesha ukiukwaji wa uhuru wa waandishi habari chini ya Serikali ya Magufuli iliyoingia madarakani mwaka 2015.


Like it? Share with your friends!

0