Marekani kuanza tena kutekeleza adhabu ya kifo


0

Serikali ya Marekani itaanza tena kutekeleza adhabu ya kifo, ambapo Mwanasheria mkuu wa Serikali ya nchi hiyo Bill Barr, ametangaza hayo jana na tayari tarehe imeshapangwa kwa watu watano waliohukumiwa kifo kuadhibiwa kwa njia hiyo.

Barr ameiagiza idara ya magereza nchini humo kutumia njia mpya ya kuwadunga wahukumiwa sindano hatari, kama njia ya kutekeleza adhabu hiyo.

Adhabu hiyo ilisitishwa nchini humo miaka 16 iliyopita. Kwenye taarifa, ya Barr imeeleza kuwa wizara ya sheria inazingatia kikamilifu utawala wa sheria na ni wajibu wake kutekeleza hukumu ambayo imetolewa kulingana na mfumo wa haki, kwa manufaa ya waathiriwa na familia zao.

Adhabu hiyo inarudishwa ikiwa wanaharakati wa haki za binadamu ulimwengu wamekuwa wakiipinga vikali, adhabu hiyo kutokana na kwamba si adhabu ya kutoa funzo, bali imekuwa ni adhabu inayokiuka haki ya mtu kuishi.

End


Like it? Share with your friends!

0