Mamilioni ya Waislam waanza ibada ya Hijja katika mji wa Makka


0

Zaidi ya mahujaji milioni 2 wamekusanyika katika mji wa Makka nchini Saudi Arabia kuanza rasmi ibada yao ya Hijja, ambayo ni nguzo moja wapo kati ya nguzo tano katika dini ya kiislamu inayowaongoza mahujaji, katika njia aliyoipita mtume Muhammad miaka 1,400 iliyopita.

Hijja katika uislamu imenuiwa kuwaunganisha waislamu wote, huku mahujaji wakijiweka mbali na utajiri na mali.

Mahujaji wanaume waliyovalia nguo nyeupe na wanawake wakivalia nguo nyeupe na kitambaa cheupe kichwani, watafanya tawaf yani kuizunguka al-kaaba mara saba

Hijja ya mwaka huu inafanyika wakati kukiwa na mgogoro wa kisiasa na wa kimadhehebu kati ya Saudi Arabia na Iran huku migogoro ikiendelea nchini Yemen, Syria na Libya.

Waislamu duniani walioko katika maeneo ambayo ni wachache pia wanakabiliwa na vitisho vinavyoongezeka,  ikiwa ni pamoja na jimbo linalodhibitiwa na India Kashmir ambako sheria ya hali ya dharura inaendelea.


Like it? Share with your friends!

0