Mamilioni waingia mtandaoni kuona Sony PlayStation 5


0

Wakati watumiaji wengi wa michezo ya PlayStation walikuwa na kiu kubwa ya kutaka kujua muonekano wa Console mpya ya PlayStation 5 maarufu kama PS5, Sony walipanga kuonesha michezo itakayoambatana na PS5 kupitia mitandao (livestream). Sony ilitangaza kuahirisha tukio lake la kuonyesha michezo ya PlayStation 5 hadi jana Juni 11.  Awali Kampuni ya mifumo ya burudani inayofahamika kama Sony Entertainment System (SES) ilipanga tukio hilo kufanyika Juni 4 lakini imelazimika kuliahirisha kutokana na hali kutokuwa shwari kufuatia kifo cha George Floyd na maandamano dhidi ya ubaguzi wa rangi  na manyanyaso ya polisi yanayoendelea sehemu mbali mbali duniani.

Katika tukio la kipekee la jana, watazamaji 11,023,583 walishuhudia maonesho ya games za PS5. Na huu ndo mwonekano mpya wa Sony PS5!

Sony ilionesha tukio hilo kwa picha ya yenye ubora wa FULL HD 1080p na si ULTRA HD 4K, kusudi kubwa ni kurahisisha utengenezaji wa video hizo kipindi hiki wafanyakazi wake wanafanyia kazi kutokea nyumbani kufuatia janga la COVID 19. Hata hivyo Sony ilisisitiza kuwa michezo iliyooneshwa siku ya Alhamisi ilikuwa bora zaidi pale mtumiaji alipotumia luninga ya 4K, 

Sony tayari wamesha taja jina la Console, Nembo na Padi ya DualSense maarufu kama DualShock5 ikiwa pamoja na baadhi ya michezo itakayo kuwemo na mapema mwezi Mei sony walitanangaza uwezo wa PS5 kucheza michezo iliyotengenezwa kwakutumia Unreal engine 5.

Sony PS5 mrithi wa Playstation 4 (PS4), itakuwa na Processor ya AMD Zen2 yenye Core nane, AMD RDNA 2 Graphic Processor, GB 16 za GDDR6 RAM na hifadhi ya SSD ya GB 825 yenye kasi ya GB 5.5 kwa sekunde. Padi ya DualSense itakuwa na haptic feedback yani mitetemo itakayotokana na jinsi itakavyo guswa, itakuwa na microphone na USB type C. Batani maarufu ya “SHARE” imebadilishwa na kuwa na jina la “CREATE” japokuwa hadi sasa bado Sony hawajasema ni nini haswa watumiaji wanaweza kufanya kupitia batani hiyo.

Tasnia ya gaming ni moja ya tasnia ya ubunifu inayoingiza pesa nyingi kwa makampuni husika. Mwaka 2018 tasnia ya michezo ya kompyuta (games) ilingiza jumla ya USD 134.9 billion, hii ni sawa na takriban shilingi za kitanzania trillion 312.3.


Like it? Share with your friends!

0