Malawi kupiga kura katika uchaguzi wa marudio Kesho


0

MALAWI

Wananchi wa Malawi kesho wanatarajiwa kupiga tena kura katika uchaguzi wa marudio ikiwa ni miezi mitano imepita baada ya mahakama ya katiba kubatilisha matokeo ya kura za Urais kufuatia malalamiko ya viongozi wa upinzani kuwa uchaguzi ulikuwa na dosari na ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi.

Rais wa nchi hiyo Peter Mutharika alitangazwa kushinda kiti cha urais kwa asilimia 38.5 ya kura zote katika uchaguzi uliofanyika mwezi May 2019.

Lakini viongozi wa vyama vya upinzani walipinga matokeo hayo katika mahakama ya kikatiba kwa madai ya kukiuka taratibu za uchaguzi.

Mwezi February, 2020 mahakama ilitoa uamuzi na kuamua kubatilisha matokeo hayo na kuagiza kurudiwa kwa uchaguzi huo.

Upinzani sasa umeungana na kusimamisha mgombea mmoja wa kuchuana na rais Mutharika ambaye anagombea kwa kipindi cha muhula wa pili katika nafasi hiyo.

Upigaji kura wa kesho umezungukwa na migogoro pamoja na mgawanyiko kwani kumekuwa na maandamano nchi nzima ya kuipinga serikali na vurgu ambazo zinatishia kuingiza malawi katika Mgogoro mkubwa.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini humo pia alijuzulu nafasi yake na kutoa nafasi kwa timu mpya ya kusimamia uchaguzi kuteuliwa.


Like it? Share with your friends!

0