Majaribio ya Hydroxychloroquine kuanza tena


0

UINGEREZA

Majaribio ya dawa yenye utata ya malaria inayotumiwa na rais wa Marekani Donald Trump Hydroxychloroquine itaanza kufanyiwa majaribio tena kuona kama inauwezo wa kutibu au kuzia kupata maambukizi ya virusi vya corona.

Kwa mujibu wa shirika la utangazaji la BBC, mchakato wa kufanya majaribio ya dawa hiyo inayofahamika kwa lugha ya kitaalamu kama COPCOV ulisitishwa kwa muda baada ya watafiti kudai kuwa dawa hiyo haikuwa na faida na inaongeza hatari kwa kusababisha mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida na kifo.

Taarifa hiyo ilisababisha Shirika la afya duniani WHO kusitisha majaribio yake ya kutibu virusi vya corona.

Lakini sasa hoja hizo zimebainika kuwa hazina vigezo watafiti wapo katika mchakato wa kuendelea kufanya utafiti kama kweli inaweza kuzuwia maambukizi au la.

Majaribio hayo yatawezesha dawa za chloroquine, hydroxychloroquine au placebo kutolewa kwa zaidi ya wahudumu wa afya 40,000 kutoka mataifa ya Ulaya, Afrika, Asia na Amerika Kusini.

Wahudumu wa afya wanatajwa huenda wakathiriwa na wimbi la pili la maambukizi linalotarajiwa kwa kiwango kikubwa katika msimu wa majira ya baridi.

Mmoja wa watafiti wakuu Prof Sir Nicholas White kutoka Chuo kikuu cha Oxford alisema Hydroxychloroquine inaweza kuzuwia maambukizi na hii itabainika kwa tafiti mbalimbali ambazo zinahitaji kuthibitishwa.

 


Like it? Share with your friends!

0