Mahujaji wazuiwa kuingia Saudia


0

SAUDI ARABIA

Saudi Arabia imepiga maarufuku raia kutoka mataifa mengine kufanya ibada ya hija nchini humo mwaka huu ili kudhibiti virusi vya corona.
Taarifa kutoka nchini humo zinaeleza kuwa ni idadi ndogo tu ya watu wanaoishi kwa sasa katika ufalme huo watakaoweza kushiriki ibada hiyo inayotarajiwa kufanyika mwishoni mwa Julai mwaka huu.
Maafisa nchini humo wanasema hii ndio njia pekee itakayowezesha kufanya mipango ya kutokaribiana ambayo itawezesha watu wawe salama.
Watu takriban milioni mbili wangeweza kutembelea mji wa Maka na Madina katika msimu wa kiangazi kwa ajili ya ibada ya hija ambayo hufanyika kila mwaka kulingana na imani ya kiislamu.
Kwa kawaida hija ni moja ya vipindi muhimu katika kalenda ya dini ya kiislamu, na pia ni mojawapo wa nguzo tano za kiislam ambayo kila Muislam mwenye uwezo na mwenye afya nzuri hutakiwa kuitekeleza walau mara moja ili kuishi maisha mazuri na uwajibikaji
Mahujaji hukusanyika mjini Maka na kusimama mbele ya Kaaba, wakimuomba Mungu kwa pamoja. Nchi hiyo imerekodi visa vya corona 161,005 na vifo vilivyotokana na ugonjwa huo ni 1,307.

 


Like it? Share with your friends!

0