Mahakama yaruhusu mshukiwa wa mauaji kumzika mumewe


0

Mahakama Kuu nchini Kenya imruhusu Sarah Wairumu Kamotho ambaye ni mke wa mfanyabishara Tob Cohen kuhudhuria mazishi ya mumewe.

Bilionea Cohen aliuawa na mwili wake kufichwa katika tanki la maji nyumbani kwake, baada ya siku 60 na mkewe anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za mauaji hayo.

Mahakama hiyo iliamuru mkuu wa Gereza la Wanawake la Lang’ata kutoa afisa mmoja ili kumsindikiza mjane huyo, kuhudhuria mazishi hayo yaliyopangwa kufanyika leo.

Ijumaa iliyopita Sarah kupitia kwa wakili wake, Philip Murgor aliwasilisha ombi lake akitaka Mahakama imruhusu kuhudhuria mazishi ya mume wake kwa kile alichodai kuwa ana haki za kufanya hivyo kwa kuwa yeye ni mke halali na Mahakama haijamtia hatiani.

Akitoa majibu ya ombi hilo leo asubuhi Jumatatu Septemba 23, Jaji Stellah Mutuku alisema “Naamuru bosi wa Gereza la Lendlelaata kuwezesha uwapo wa Wairimu kwenye mazishi ya Cohen.

Awali wakili George Ouma ambaye leo alisisimama mahakamani kwa niaba ya wakili wa mjane huyo, alisema wanafamilia wote walifanya mkutano na kukubaliana kuwa Sarah aruhusiwe  kuhudhuria katika mazishi hayo ya mumewe yaliyopangwa kufanyika katika makaburi ya Wayahudi kando ya Barabara ya Wangari Maathai, Nairobi leo Jumatatu mchana.

“Tumekubaliana na wakili wa familia Cliff Ombeta kwamba Sarah aruhusiwe kuhudhuria mazishi ya marehemu mumewe,” alisisitiza wakili Ouma na kuongeza kuwa kwa upande wake anaamini kwamba haitakuwa vibaya kwa mjane huyo kuhudhuria mazishi hayo.

Kwa upande wake wakili huyo wa familia, alisema wamekubaliana kwamba hakuna haja ya kujihusisha na mzunguko mpya  wa kisheria.

“Tulikutana Septemba 19 kabla ya maombi haya na tulikubaliana kwamba hakuna haja ya kuwa na vitambulisho vya vita juu ya mahudhurio. Hakuna mali katika maiti,” alisisitiza wakili Ombeta.

Kufuatia kauli hiyo, mwendesha mashtaka wa Serikali, Nicholas Muteti alisema Serikali haina pingamizi dhidi ya maombi hayo.

“Lengo letu ni kuwezesha na si vinginevyo, kama kuna makubaliano hapo hatuna pingamizi,” aliongeza Muteti.

Akisoma uamuzi huo, jaji Mutuku alisema pande zote zimefanya kazi ya Mahakama kuwa rahisi kutokana na kukubaliana na suala hilo.

“Katika mazingira hayo, korti hii inaamuru Gereza la Wanawake wa OC Liongoata limpeleke Sarah Wairimu kuhudhuria mazishi ya marehemu mumewe kwenye Makaburi ya Wayahudi leo saa 2.00 jioni,” jaji Mutuku alielekeza upande wa mashtaka.

Baada ya uamuzi huo, wakili Ombeta alisema hii ni kesi ya kwanza ambayo mtuhumiwa wa mauaji anasindikizwa ili kuhudhuria mazishi ya mtu anayetuhumiwa kumuua.

Wakili huyo alisema mazishi hayo pia yatahudhuriwa na dada wa bilionea huyo, ambaye kwa sasa yuko nje ya nchi ambako kaka wa mfanyabiashara huyo Bernard Cohen ndiye aliyepewa jukumu la kusimamia mazishi hayo yatakayofanyika kwa mujibu wa taratibu

 


Like it? Share with your friends!

0