Mahakama yakataa ombi la CHADEMA


0

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeyakataa maombi ya udhuru ya washitakiwa Ester Matiko na Vicent Mashinji yaliyowasilishwa mahakamani hapo jana, kutaka kesi hiyo iahirishwe.

Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Thomas Simba, amesema sehemu kubwa ya washitakiwa ni wabunge hivyo kitendo cha kuwaruhusu kutoka nje ya nchi kitachelewesha kesi hiyo.

Jana, upande wa utetezi uliiomba Mahakama kuahirisha kesi hiyo kwa sababu ya dharura ya washtakiwa hao kwa vile Mashinji anahudhuria kesi ya uchochezi inayomkabili kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Songea, wakati Matiko amealikwa kwenda Kigali Rwanda, Septemba 25 hadi 28 na kwamba kati ya Oktoba 13 na 18 atakuwa anahudhuria Bunge la Umoja wa Ulaya kama Mjumbe wa Afrika.

Katika uamuzi wa jana, Hakimu Mkazi Mkuu Simba ameikubali hati iliyowasilishwa kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Songea inayoonesha mshitakiwa Mashinji kuhudhuria mahakamani hapo.

Mahakama imeiahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 10 mwaka huu, ili kuwapa nafasi upande wa utetezi kujiandaa na utetezi wao,

 


Like it? Share with your friends!

0