Uncategorized

Magufuli aweka Jiwe la msingi Ujenzi wa Mahandaki ya reli ya SGR


0

Morogoro, Tanzania

Rais Dkt John Pombe Magufuli ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa Mahandaki manne yenye urefu wa kilometa 2.7 katika reli ya kisasa kutoka Morogoro hadi Makutupora.
Mahandaki hayo yatatumika kupitisha reli ambayo inagharimu kiasi cha shilingi Trillioni 6.05
Akizungumza na wananchi wa Kilosa wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi, Rais Magufuli amesema kuwa wapo waliomuona anaota aliposema nataka kujenga reli lakini amefanikiwa kwa kutumia fedha za ndani
“Tanzania sisi sio masikini, mradi huu (SGR) tunajenga kwa fedha zetu zaidi ya Tsh TrilION 6. 05 hivyo tutembee kifua mbele kwa kuweza kujenga mradi huu wa kihistoria” alisema Rais Magufuli.

Amewataka viongozi wote wanaohusika kuanzisha korido za kiuchumi katika maeneo yote ya reli ili wananchi wafanye shughuli za kiuchumi katika maeneo hayo kwani ni fursa kwa kufanya uwekezaji wa vitu mbalimbali.
Pia ametoa rai kwa Makandarasi wazalendo kufanya kazi kwa kujituma kwani kwa sasa hafurahishwi na utendaji kazi wa wanaojenga barabara ya Kilosa – Dumila.
“wametumia muda mrefu kujenga barabara hii, nataka huu mradi ubadilike hivyo nawapa mwezi mmoja kazi zianze kufanyika” alisema Rais Magufuli
Mbali na hayo amesema anatambua matatizo yanayowakumba watu wa maeneo hayo yaliyopita ujenzi wa reli hiyo ikiwemo migogoro ya ardhi na wameshafuta mashamba zaidi ya 49 ambayo yalichukuliwa na matajiri na yatagawiwa kwa wananchi maskini.
Rais John Magufuli yupo mkoani Morogoro kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi na kuzindua miradi mbalimbali inayoendelea kujengwa katika mkoa huo.


Like it? Share with your friends!

0