Magufuli ateua wakuu wa mikoa 2 na wakuu wa wilaya 9


0

TANZANIA

Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli leo amemteua Dkt. Philemon Sengati kuwa mkuu wa mkoa wa Tabora akichukua nafasi ya Aggrey Mwanri ambaye amestaafu na Thobias Andengenye kuwa mkuu wa mkoa wa Kigoma akichukua nafasi ya Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga ambaye naye amestaafu.

Katika taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa mawasiliano Ikulu, Rais Magufuli pia amefanya uteuzi wa wakuu wa wilaya tisa akiwemo kamishna msaidizi mwandamizi wa magereza (SACP) Ismail Twahir Mlawa amabaye ameteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro kuchukua nafasi ya James Mugendi Ihunyo ambaye amestaafu.

Aliyekuwa katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dodoma, Jamila Yusuf ameteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Mpanda mkoani Katavi anachukua nafasi ya Lilian Charles Matinga ambaye amestaafu.

Mhandisi wa wizara ya ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Martine Ntemo kuanzia sasa atakuwa mkuu wa wilaya ya kibaha mkoani Pwani akichukua nafasi ya Asumpter Nshunju Mshama ambaye amestaafu.

Pia amemteua Salum A. Kali kuwa mkuu wa wilaya ya Magu mkoani Mwanza, Kabla ya uteuzi huo Kali alikuwa Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Mwanza na anachukua nafasi ya Dkt. Philemon Sengati ambaye ameteuliwa kuwa mkuu wa Mkoa wa Tabora.

Rais Magufuli pia amemteua katibu tawala wa wilaya ya Singida Wilson Samwel Shimo kuwa mkuu wa wilaya ya Nyang’wale mkoani Geita, Kabla ya uteuzi huo Shimo alikuwa katibu tawala wa wilaya ya Singida.


Kanali Mathias Kahabi ameteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera akichukua nafasi ya Saada Malunde ambaye amestaafu.

Abbas Kayanda aliyekuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Karatu ameteuliwa sasa atakuwa mkuu wa wilaya ya Karatu mkoani Arusha akichukua nafasi ya Theresia Jonathan Mahongo ambaye amestaafu

 

Rais Magufuli pia amemteua Lazaro Jacob Twange kuwa mkuu wa wilaya ya Babati Mkoani Manyara anachukua nafasi ya Elizabeth Simon Kitundu ambaye amestaafu.

Na Toba Alnason Nguvila ameteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Handeni akichukua nafasi ya Godwin Gondwe ambaye amehamishwa kituo cha kazi na kuwa mkuu wa wilaya ya Temeke, Dar es Salaam baada ya Felix Jackson Lyaniva kustaafu.
Kabla ya uteuzi huo, Nguvila alikuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Longido Mkoani Arusha.

Uteuzi wa viongozi hao umeanza leo tarehe Julai 03, 2020 na wateule wote wanatakiwa kuwepo Ikulu, Chamwino mkoani Dodoma siku ya Jumatatu Julai 6, 2020 saa 4:00 asubuhi.


Like it? Share with your friends!

0