Magereza ya Kigoma yaongoza kuwa wakimbizi


0

Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imesema magereza ya mkoa wa Kigoma yanaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya wafungwa na mahabusu ambao ni wakimbizi kutoka nchi mbalimbali.

Hayo yameelezwa bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhandisi Hamad Masauni, wakati akijibu swali la mbunge wa Viti Maalum(CUF) Rukia Kassim Ahmed, aliyetaka kujua mpango wa Serikali katika kuwarudisha nchini mwao wafungwa na mahabusu ambao ni wakimbizi, ili kupunguza msongamano katika magereza hapa nchini.

Akijibu swali hilo Naibu Waziri Masauni amesema, ni kweli idadi wa wafungwa na mahabusu ambao ni wakimbizi ni kubwa lakini mkoa wa Kigoma unaongoza kwa kuwa na wafungwa na mahabusu hao 91, ambapo kati ya hao 38 ni wafungwa na mahabusu 53.

Hata hivyo Masauni amesema Serikali imeendelea kuwarudisha nchini mwao wafungwa hao kwa siri pindi wamalizapo vifungo vyao, lakini pia wakimbizi wameendelea kurudishwa katika nchi zao kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Wakimbizi na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji.

Kuanzia mwezi Julai 2018 hadi mwezi april 2019, jumla ya wakimbizi 31643 kutoka Burundi walirejeshwa nchini mwao kwa hiari yao, zoezi ambalo linatajwa kuongeza jumla ya wakimbizi waliorudishwa nchini mwao tangu mwaka 2017 hadi 2019 kufikia 66148.


Like it? Share with your friends!

0