Madhara ya COVID – 19 kwa chanjo ya watoto


0

CHANJO

Shirika la Umoja wa Mataifa la Watoto (Unicef), Taasisi ya Chanjo na Shirika la Chanjo la Gavi, yameonesha wasiwasi kuwa maelfu ya watoto wanaweza kupoteza maisha kutokana na maradhi yanayozuilika, baada ya kukatizwa kwa programu za chanjo kutokana na virusi vya corona.

Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), kiasi cha nchi 68 duniani zimeathirika baada ya kusitisha kampeni za chanjo.

Shirika la Afya Duniani (WHO) lilishauri nchi nyingi kusitisha chanjo, ili kusaidia kudhibiti kuenea kwa virusi vya corona.

Baadhi ya wataalamu wanabashiri uwezekano wa kuibuka madhara ya muda mrefu kutokana na hatua hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Unicef, Henrietta Fore, anasema suala hilo litaleta shida baadaye, kwani kwa sasa surua ipo kwa kiwango cha juu, kuhara na kipindupindu.

 

Anasema wamejitahidi kupambana na maradhi mengi yanayozuilika kwa watoto, lakini upo wasiwasi kwamba hiyo yote ilikuwa kazi bure kwani magonjwa yanaweza kuanza tena.

Katika mtandao wa BBC wameandika kuwa, kuna sababu kadhaa ya huduma ya chanjo kuvurugwa kipindi hiki, ikiwemo wazazi kuhofia kupata maambukizi ya Covid-19 watakapotoka nje ya nyumba zao.

 

 


Like it? Share with your friends!

0