Maandamano ya Marekani ‘yatapakaa’ Duniani


0

Maandamano ya kupinga mauaji ya Mmarekani mweusi, George Floyd, yamegusa hisia za watu tofauti duniani, wanaoyaunga mkono.

Mkuu wa sera ya kigeni wa Umoja wa Ulaya (UN), Josep Borrel, amesema kifo cha Floyd ni matokeo ya matumizi mabaya ya madaraka.

Borrel amekaririwa na chombo cha habari cha cha ujerumani Doch Welle siku ya jana akisema kwamba kama ilivyo kwa Wamarekani, UN pia imeshtushwa na kifo hicho kilichotokana na kukandamizwa shingoni kwa goti na askari polisi Mmarekani mweupe; kwa zaidi ya dakika nane hadi alipoacha kupumua.

Amesema maafisa wanaosimamia utekelezaji wa sheria hawapaswi kutumia mamlaka yao vibaya kama iliyotokea na kusababisha kifo cha Floyd, hivyo inapaswa kulaaniwa duniani kote.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Heiko Maas, amesema katika mkutano na Waziri mwenzake wa Ukraine, Dmytro Kuleba, kwamba Floyd aliuawa kikatili na kwamba maandamano yanayoendelea Marekani yanaeleweka na ni zaidi ya uhalali.

Hata hivyo, Maas ameepuka kuilaumu moja kwa moja serikali ya Marekani kwa namna ilivyoshughulikia maandamano na ukandamizaji wa polisi dhidi ya washiriki wa maandamano hayo.

Badala yake amesema kila kitendo cha vurugu kinastahili kuchunguzwa, na kwamba waandishi wa habari wanapaswa kuruhusiwa kufanyakazi kwa uhuru.

 

Maandamano yanaendelea kufanyika katika miji mengine duniani ikiwemo Sydney, ambako waandamanaji wamekuwa wakirudia maneno ya “siwezi kupumua” yakiwa ni maneno ya mwisho kabla mauti kumfika Floyd.

Rais wa Ghana Nana Akufo-Ado, amesema si sahihi katika karne ya 21, taifa kubwa la kidemokrasia kama Marekani kuwa linapambana na kadhia ya ubaguzi wa kimfumo na kwamba hakutarajia kama mauaji ya kikatili yanaweza kutokea kwenye nchi hiyo.

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga, ameomba kuwepo sala ya kuombea haki na uhuru kwa raia wa Marekani.

Waziri wa Fedha wa Afrika Kusini, Tito Mboweni, amekumbuka kuongoza kundi dogo la waandamanaji nje ya ubalozi wa Marekani miaka kadhaa iliyopita, kupinga mauaji ya dhahiri ya watu weusi.

Mboweni amesema balozi wa Marekani wakati huo, Patrick Gaspard, alimualika ofisini kwake na kumuambia kwamba “unachokiona si chochote, hali ni mbaya zaidi.”

 

 

 


Like it? Share with your friends!

0