Uncategorized

Maambukizi ya corona yafikia milion 10


0

Zaidi ya watu laki tano wamefariki dunia kutokana na maambukizi ya virusi vya corona yanayosababisha COVID – 19, huku maambukizi hayo yakifikia milioni 10 tangu kulipuka kwake nchini China mwishoni mwa mwaka jana.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Chuo Kikuu cha Johns Hopkins (JHU), Marekani imeendelea kuongoza kwa visa vingi vya maambukizi baada ya watu milioni mbili kukutwa na virusi hivyo huku vifo vikiwa ni 125,000.

Kituo cha Afrika cha kudhibiti na kuzuia magonjwa kimesema visa vya maambukizi ya COVID-19 vimeongezeka barani Afrika, ambapo mpaka sasa kuna jumla ya maambukizi 371,000 na vifo 9,484.

Shirika la habari la China (Xinhua) limeripoti kuwa China imeweka vizuizi katika miji inayozunguka mji wa Beijing ili kuzuia wimbi jipya la maambukizi ya corona, huku mamlaka zikionya kuwa mlipuko huo bado ni mkubwa na mgumu.

Kutokana na kuongezeka kwa visa hivyo wasiwasi umeenea katika mataifa mbalimbali ambapo Marekani imesitisha mpango wake wa kulegeza masharti katika majimbo 12 yaliyotaka kuondoa amri ya kutotoka nje.

 

 


Like it? Share with your friends!

0