Uncategorized

Liverpool ‘baba lao’ EPL


0

UINGEREZA

Ni dhahiri kwamba baada ya miaka 30 ya kuusaka ubingwa wa soka katika Ligi Kuu ya Uingereza (EPL), hatimaye timu ya Liverpool yenye Makao Makuu yake huko ?Merseyside, imelitwaa taji hilo lenye heshima, hadhi na thamani kubwa zaidi katika soka nchini humo.

Ushindi huo kwa Liverpool iliyoanzishwa mwaka 1892 unapatikana baada ya timu ya Chelsea kupata ushindi wa bao 2-1 jana, dhidi ya Manchester City katika kabumbu lililosakatwa kwenye dimba la Stamford Bridge.

Wakati Chelsea ikiutumia mgongo wa Manchester City – waliokuwa wanautetea ubingwa huo; kuifanya Liverpool kuwa mabingwa, vinara hao wa soka wanaonolewa na Kocha nguli, Juergen Klopp, jumatano iliyopita iliibamiza Crystal Palace kwa goli 4 – 0 na kuchukua uongozi wa ligi hiyo kwa pointi 23; hivyo ikaiombea mabaya Manchester City iliyokuwa ya pili, ipigwe na Chelsea, ili itangazwe bingwa, huku ikiwa na mechi saba kabla ya kukamilika kwa ligi hiyo.

Mashabiki wa Liverpool maarufu kama (The Reds ), siku ya jana walipuuza vizuizi vilivyoweka kukabiliana na janga la corona na walikusanyika nje ya uwanja wa Anfield kusherekea ushindi wa timu yao ikiwa ni baada ya kuukosa ubingwa huo kwa kipindi kisicho pungua miaka 30.

Kocha Mkuu, Klopp alionekana kujawa na hisia za furaha ambapo aliongea katika chombo cha habari cha Sky Sports akisema, “sina maneno ya kuelezea, siamini. Ni zaidi ya vile nilivyofikiria kwamba inawezekana kuwa mabingwa na klabu hii ni jambo la kufurahisha…”

Akaongeza, ”sijawahi kusubiri miaka 30, nimekuwa hapa kwa miaka minne na nusu, lakini ni mafanikio makubwa, hususan baada ya likizo ya miezi mitatu kwa sababu hakuna mtu aliyejua kwamba tutatawazwa washindi.”

Hata hivyo, kutokana na masharti yaliyowekwa kukabiliana na virusi vya corona, the reds hawataweza kusherehekea ushindi huo uliosubiriwa kwa muda mrefu na kama ilivyo kawaida yao katika kushabikia.

Baada ya ushindi huo wa Chelsea, Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola aliwapongeza Liverpool kwa kushinda taji hilo.

“Kushinda taji hilo ndio lililokuwa lengo la Liverpool ambayo ilikuwa imesubiri kwa muda mrefu ili kutawazwa mabingwa tena, baada ya kushinda taji hilo mara 11 kati ya mwaka 1973 na 1990,” amesema.

Chanzo BBC SWAHILI & DW.


Like it? Share with your friends!

0