LIVE | Fuatilia mjadala kuhusu VIKOBA na Uchumi wa Wanawake.


0

Wakati maadhimio ya usawa wa kijinsia yakiendelea kupiganiwa dhidi ya wanawake, maadhimio hayo hivi sasa yanaanza kuonesha matumaini baada ya uwepo wa wanawake wengi kujishughulisha na shughuli mbalimbali ambazo huko nyuma mara nyingi zimekuwa zikifanywa na wanaume.

Lissa Seka na Salome Peter, ni miongoni mwa wanawake ambao hawakusubiri fursa ziwafate mikononi na wameamua kufanya shughuli zinazofanywa na wanaume kuonyesha kwamba hakuna kazi ambayo mwanamke akipewa fursa atashindwa kuifanya licha ya uwepo wa changamoto za hapa na pale.

Lakini pia kwa namna gani wanawake hawa wanatumia taasisi za kifedha kama Vicoba kuendeleza shughuli zao?

Wiki hii katika kipindi cha Ongea na Shangazi, kimezungumza na wanawake hawa, Je unatamani kujua ni kazi zipi za kiume lakini wao wameamua kuzifanya bonyeza video hapa chini ufatilie mjadala huu ambao umeongozwa na Shangazi Maria Sarungi


Like it? Share with your friends!

0