Kwanini eneo duni la Dharavi nchini India Limemudu mapambano dhidi ya COVID 19


0

INDIA

Wakati nchi ya India ilipodai kupata mgonjwa wa kwanza mwenye maambukizi ya virusi vya corona kutoka katika eneo lenye makazi duni la Dharavi Mwezi April mwaka huu, wengi walihofia kuwa ugonjwa huo ungegeuza barabara zake kuwa sehemu ya makaburi kwani kanuni ya kukaa umbali wa mita kadhaa ilikuwa ni ngumu kutekelezeka.

Lakini baada ya miezi mitatu, maofisa wa eneo hilo wanatoa matumaini kwa wananchi kuwa maambukizi mapya yanaanza kushuka.

Kwa mujibu wa shirikala habari la AFP, Afisa wa jiji Kiran Dighavkar, anasema wanashukuru kwa sheria kali walizojiwekea katika kuzuia kuenea kwa virusi hivyo .

Eneo hilo la makazi duni linakadiriwa kuwa na watu millioni moja na wengi wao wanafanya kazi katika viwanda au wafanyakazi wa majumbani na madereva kwa waajiri wao wanaoishi eneo tajiri Mumbai.

Baadhi ya wakazi wa Dharavi hulala chini katika chumba kimoja na mamia wanatumia choo cha pamoja. Mamlaka zilitambua mapema kuwa mazoea yakawaida yataendelea kutumika licha ya hatari ya COVID 19.

“kukaa umbali wa mita kadhaa, kujitenga majumbani na kutoshikana ni vitu ambavyo havikuwezekana kabisa kwani watu wengi wanatumia vyoo vya pamoja” alisema Dighavkar

Mpango wa awali wa kupita nyumba kwa nyumba kufanya vipimo vya uchunguzi kwa wakazi wa eneo hilo ulishindikana kutokana na joto kali hali iliyokuwa ikisababisha wahudumu wa afya kukosa hewa wakiwa na mavazi ya kujikinga na maambukizi hayo.

Maambukizi yalianza kuongezeka kwa haraka na watu chini ya 50,000 ndio walikuwa wamepimwa kama wanadalili hivyo maafisa walitakiwa kuongeza juhudi na kuja na ubunifu.

Hivyo kila siku wahudumu wa afya walitengeneza kambi maalumu katika sehemu tofauti tofauti za eneo hilo na wananchi walitakiwa kufika kwa ajili ya uchunguzi wa afya zao na kama mtu ataonesha dalili zozote basi atapimwa COVID 19. Maeneo ya Shule, kumbi za harusi na viwanja vya michezo zilibadilishwa kuwa Karantini ambazo zilitoa chakula bure, dawa za vitamini na mda wa mazoezi ya yoga.

Hatua kali za kupunguza maambukizi ziliwekwa katika nyumba za watu 125,000 ikiwemo matumizi ya drones kufuatilia mienendo ya watu na tahadhari ya polisi huku jeshi kubwa la kujitolea likisambaza chakula.

Mwishoni mwa mwezi June zaidi ya nusu ya watu wanaoishi kwenye makazi hayo duni walikuwa wamechunguzwa kuona kama wanadalili zozote na karibu watu 12,000 walipimwa virusi vya corona.

Mpaka sasa eneo la Dharavi limeripoti vifo 82 pekee ambao ni sehemu ya watu 4,500 waliofariki kwa maambukizi ya virusi vya corona katika mji wa Mumbai.

Madaktari wanaotoa huduma katika eneo hilo wanasema wanajiona kama wshindi lakini anasisitiza kuwa tahadhari ziendelee kuchukuliwa kwani idadi ya maambukizi inaweza ikapanda.

Changamoto itakuja pale ambapo viwanda vitaanza kufunguliwa tena ili kurudisha hali ya uchumi uliosimama kutokana na janga la virusi vya corona. Miji ya Mumbai na Delhi imekuwa ikihangaika namna ya kuwahifadhi wagonjwa wa COVID 19 wakati huu ambao visa vya maambukizi nchini india vikiongezeka kwa kasi ambapo mpaka sasa kuna visa 586,956 na vifo 17,417.


Like it? Share with your friends!

0