Kwa heri Mugabe, muasisi wa Zimbabwe


-1
-1 points

Rais wa zamani wa Zimbabwe ambaye ni muasisi na Baba wa Taifa hilo, Robert Mugabe amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 95.  Alikuwa amelazwa hospitalini nchini Singapore kwa miezi mitano.

Robert Mugabe ambaye alitawala Zimbabwe tangu uhuru wa nchi hiyo mnamo mwaka 1980, afya yake ilianza kuzorota tangu alipoondolewa madarakani na kulazimika kwenda nchini Singapore kwa matibabu.

Viongozi mbalimbali duniani wanamkumbuka Mugabe kwa namna tofauti kifo chake kimewafanya viongozi hao kumuona kama jemedali wa siasa na mkombozi wa Zimbabwe.

Rais wa sasa wa Zimbabwe amethibitisha kifo cha muasisi huyo wa uhuru wa taifa hilo, kupitia ukurasa wake wa TWITTER.

“Ni kwa huzuni mkubwa ninatangaza kifo cha baba wa taifa na muasisi wa uhuru wa Zimbabwe na rais wa zamani, kamanda Robert Mugabe,” Rais wa sasa wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa, ameandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa twitter.

Salam za pole zimeendelea kutolewa na viongozi nchi mbalimbali akiwemo Rais wa Tanzania Dk John Magufuli Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta

 

Lakini Robert Mugabe ni nani

 

Robert Mugabe alizaliwa tarehe 21 mwezi Februari mwaka wa 1924 katika kijiji kilichokuwa karibu na mji mkuu wa sasa ambao ni Harare,  wakati huo ukijulikana kama Salisbury.

Alisomea taaluma ya ualimu na anaaminika kuwa na jumla ya shahada saba kutoka vyuo vikuu.

Mke wake wa kwanza, Sally Hayfron, mzawa wa Ghana, alifariki mnamo mwaka wa 1992 kutokana na ugonjwa wa figo.

Mugabe alimuoa mkewe wa sasa, Grace Mugabe, mnamo mwaka wa 1996.

Mwanasiasa huyo alipata umaarufu mkubwa kwa mara ya kwanza pale alipoongoza vita vya msituni dhidi ya wakoloni walioitawala Zimbabwe, wakati huo ikijulikana kama Rhodesia.

Mugabe alikamatwa na kufungwa jela kwa kipindi cha miaka kumi kufuatia hotuba aliyoitoa manamo mwaka wa 1964, iliyowagadhabisha wakoloni ambao waliitaja kuwa ya uchochezi.

Aliachiliwa kutoka jela mnamo mwaka wa 1974 na kuingia kwenye siasa za kushinikiza Waingereza kusitisha utawala wake kwa Rhodesia.

Baadaye Mugabe alitor

okea nchi jirani ya Msumbiji na kurudi Rhodesia mnamo mwaka wa 1979.

Baada ya Zimbabwe kupata Uhuru wake mwaka wa 1980, Mugambe alichuka nafasi ya waziri mkuu, na kuendelea kuongoza nchi hiyo chini ya chama tawala cha Zanu PF.

Katika miaka ya mwanzo wa uongozi wake, Mugabe alisifika kwa upanuzi wa miundo msingi na huduma za kijamii, zikiwepo hospitali na shule za nchi hiyo.

Hata hivyo  alishutumiwa kwamba aliwanyanyasa wapinzani wake, wakiongozwa na kiongozi wa upinzani wa wakati huo, Joshua Nkomo.

Tume ya kanisa katoliki kuhusu haki na amani ilitoa ripoti iliyodai kwamba Zaidi ya watu 20,000 walipoteza maisha yao chini ya utawala wa Mugabe.

Mugabe alichukua wadhifa wa urais mnamo mwaka wa 1987 baada ya nafasi ya waziri mkuu kuondolewa rasmi.

Tangu wakati huo ameshinda uchaguzi mara nyingi licha ya kutajwa na wapinzani wake na waandgalizi mbali mbali kama uliojawa na udanganyifu na usiokuwa wa haki na kweli.

 

Waswahili wanasema hakuna marefu yasiyo na ncha mwisho wa Mugabe ukawadia mnamo mwaka  2017 Novemba 14, kiongozi huyo wa zamani alingo’lewa madarakani kwa shinikizo la makamu wake wa Rais akisaidiana na Jeshi la nchi hiyo.

Baada ya kungo,olewa madarakani hali ya Maisha kwa Mugabe ilionekana kuwa si nzuri kwa mujibu w a vyanzo mbalimbali vya habari vilivyokwa vikiripoti, hali ambayo ilimfanya Mugabe kupiga mnada mali zake kutokana na madeni yaliyokuwa yakimuandama.

Wakososaji wa rais huyo wametaja hatua yake ya mageuzi juu ya umiliki wa ardhi kama moja ya masuala muhimu yaliyochangia hali ya kuzorota vibaya kwa uchumi wa nchi hiyo.

Aidha, mwanasiasa huyo mkongwe amekosolewa kwa kile wapinzani wake wamekiita kukatalia madarakani, kuwanyanyanyasa wapinzani wake wa kisiasa, kumfuta kazi makamu wake na kuunga mkono azima ya mkewe ya kutaka kuwa rais wa Zimbabwe, kati ya mambo mengine yaliyozua utata.


Like it? Share with your friends!

-1
-1 points