Kusafirisha mkaa mwisho Kg 50


1
1 point

Kuanzia sasa watakaosafirisha mkaa unaozidi kilo 50 kwa matumizi ya nyumbani, watapaswa kupita katika njia na vituo vilivyoainishwa kwa ukaguzi wa bidhaa hiyo, huku wakibanwa sawa na wale wanaosafirisha nishati hiyo kwa biashara.

Hayo yamo katika kanuni za uvunaji na usafirishaji wa mazao ya misitu, ambazo zinatafsiri mkaa kwa matumizi ya nyumbani kuwa ni ule usiozidi kilo 50.

Kwa mujibu wa kanuni hizo, mkaa unapaswa kusafirishwa kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa 12 jioni. 

“Mtu yeyote anayesafirisha magogo, mbao, miti, nguzo au mkaa, isipokuwa mkaa kwa ajili ya matumizi ya nyumbani, atapaswa kupita katika njia na vituo vilivyowekwa kwa ajili ya ukaguzi,” inasomeka sehemu ya kanuni hizo.

Kanuni hizo zilizotangazwa Mei 24, mwaka huu kupitia Tangazo la Serikali namba 417, zimegawanyika katika vipengele 24 vikiwamo kamati za mavuno, kazi za kamati za wilaya, mikutano ya kamati, maombi ya uvunaji, aina za uvunaji, utunzaji kumbukumbu na uzalishaji wa mkaa.

Vipengele vingine vinahusu kusitisha kibali cha uvunaji misitu, uvunaji magogo, mbao, mkaa kwa matumizi ya biashara, uvunaji magogo, mbao, mkaa kwa matumizi ya nyumbani, muda wa usafirishaji, usafirishaji magogo, mbao, mkaa kwa matumizi ya nyumbani, kuuza katika maeneo yasiyosajiliwa na usafirishaji mkaa nje.


Like it? Share with your friends!

1
1 point