Korea Kaskazini yarusha makombora


0

Jeshi la Korea Kusini limesema kuwa Korea Kaskazini imerusha vifaa viwili ambavyo havikutambuliwa katika bahari, masaa machache baada ya nchi hiyo kutoa pendekezo la kuanzisha mazungumzo ya kidiplomasia ya kinyuklia na Marekani lakini ikaonya kuwa shughuli zake na Marekani huenda zikafikia kikomo bila ya mapendekezo mapya.

Hatua hiyo ya Korea Kaskazini na matakwa ya mapendekezo mapya yamelenga kuishinikiza Marekani kufikia makubaliano wakati mazungumzo kati yao yatakaporejelewa tena. Inaaminika kuwa Korea Kaskazini inaitaka Marekani kuipa hakikisho la usalama na afueni ya vikwazo vinavyoongozwa na Marekani kwa taifa hilo kupunguza hatua zake za kinyuklia.

Jeshi la Korea Kusini limesema litafuatilia uwezekano wa majaribio zaidi lakini halikutoa habari zaidi kuhusu vifaa vilivyorushwa na Korea Kaskazini.


Like it? Share with your friends!

0