Korea Kaskazini wajisifu kumaliza COVID 19


0

KOREA KASKAZINI

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-Un ameipongeza nchi yake kwa mafanikio waliyopata katika kukabiliana na virusi vya corona na amewaonya wasaidizi wake kwa kulegeza masharti ya tahadhari mapema.

Kim ameongea hayo katika mkutano wa kamati kuu ya watunga sera wa Chama tawala cha kikomunisti -politburo na kudai kuwa wameweza kuzuia virusi kusambaa na wamefanikiwa kudhibiti hali hiyo.

Kwa mujibu wa shirika la utangazaji la BBC, Korea Kaskazini ilifunga mipaka yake na kuwaweka maelfu ya watu karantini kwa miezi sita iliyopita wakati virusi vinaenea duniani.

Nchi hiyo inadai haijawahi kuwa na kisa hata kimoja cha COVID 19 ingawa wachambuzi wanasema ni suala ambalo haliwezekianiKim anasema licha ya mafanikio hayo makubwa yaliyowezeshwa na uongozi wa kamati kuu ya chama chake, kuna umuhimu wa kuendelea kuchukua tahadhari bila kupumzika kwani virusi vipo katika nchini za jirani

Katika picha zilitolewa na chombo cha habari cha serikali nchini humo zinazonesha maafisa wakiwa wamekaa katika mkutano huku kukiwa hakuna tahadhari yoyote iliyochukuliwa ikiwemo kukaa kwa umbali wa mita kadhaa na kuvaa barakoa.

lakini katika mitaa mbalimbali ya Pyongyang Raia wengi wameonekana kufuata kanuni za kujikinga na ugonjwa huo kama vile kuvaa barakoa na kutokusogeleana.

 


Like it? Share with your friends!

0