Korea Kaskazini imeilaumu Marekani kwa kuchochea mivutano ya kijeshi


0

Korea Kaskazini imeilaumu Marekani kwa kuchochea mivutano ya kijeshi kutokana na kufanya mazoezi ya kijeshi pamoja na Korea Kusini na kusema kuwa  itachukua hatua za kujihami.

Balozi wa Korea Kaskazini mjini Geneva, amewaambia wajumbe kwenye mkutano juu ya kupunguza silaha unaodhaminiwa na Umoja wa Mataifa, kwamba Korea Kaskazini itazifikiria upya hatua ilizochukua hadi sasa.

Hata hivyo, mjumbe wa Marekani kwenye mkutano huo, Robert Wood, ameyakanusha madai hayo kwa kusema kuwa Marekani haichochei mivutano.

Bwana Wood ameeleza kuwa Marekani inadhamiria kulitekeleza lengo la kuondolewa silaha za nyuklia za Korea Kaskazini kama jinsi kiongozi wa nchi hiyo, Kim Jong Un, alivyokubaliana na Rais Donald Trump kwenye mkutano wao wa kwanza uliofanyika Singapore mwaka uliopita.

Mjumbe huyo wa Marekani amesema nchi yake inasubiri kwa hamu kubwa, kurejea kwenye mazungumzo na Korea Kaskazini ili kulitekeleza lengo lililowekwa kwenye mkutano huo.


Like it? Share with your friends!

0