Kipindupindu chaibuka upya Dar


0

Ugonjwa wa kipindupindu umeibuka tena katika Manispaa ya Ilala jijini Dar es salaam, baada ya kugundulika kwa mgonjwa mmoja ambaye alilazwa katika Zahanati ya Vingunguti.

Kaimu Meya wa Wilaya ya Ilala, Omari Kumbilamoto amesema hadi sasa wamebaini chanzo cha ugonjwa huo kuwa ni baadhi ya wananchi kutiririsha majitaka, ambayo yanakwenda kwenye maji yanayotumiwa na wananchi.

Katika kuhakikisha ugonjwa huo hauendelei kuwapata watu wengine Kumbilamoto amesema kwa sasa wametenga eneo maalum la kuwahudumia wagonjwa wa kipindupindu, lakini pia kuchukua tahadhari endapo kutakua na ongezeko la wagonjwa hao.


Like it? Share with your friends!

0