Kajange: Malaria bado ni tishio


0

Mratibu wa malaria kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Stella Kajange, amesema ugonjwa wa malaria umepungua kwa asilimia 50, ikiwamo kupungua pia kwa maambuzi na vimelea vya ugaonjwa huo kwa asilimia 15 kwa mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 7.3 kwa mwaka 2018.

Alisema Tanzania inaendelea vizuri katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo ambao umekuwa  ni tishio kwa jamii.

“Licha ya kupungua kwa ugonjwa huu nchini lakini ugonjwa huu bado ni tishio kwa jamii na hivyo Serikali inaendelea na utekelezaji wa afua mbalimbali ili kuhakikisha tatizo hilo linapungua,” alisema Kajange

Aidha aliongeza  kuwa sera ya mwaka 2007, inaelezea muelekeo wa nchi katika kuhakikisha kuwa wananchi wanakuwa na afya njema ili waendelee na shughuli zao mbalimbali za uzalishaji na kujipatia kipato.

Ugonjwa wa malaria umetajwa kuwaathiri zaidi Watoto wadogo wenye umri wa chini ya miaka mitano na wajawazito licha ya jitihada mbalimbali za kukabiliana na ugonjwa huo.


Like it? Share with your friends!

0