Kadinal ashtakiwa kwa unyanyasaji wa kingono


0

Kadinali George Pell wa Kanisa Katoliki nchini Australia amekutwa na hatia za unyanyasaji wa kingono dhidi ya watoto, baada ya kufunguliwa mashataka tangu mwezi Desemba 2018.

Pell mwenye umri wa miaka 77, anadaiwa kuwafanyia unyanyasaji vijana wawili mwaka 1996, huku yeye akikana kuhusika.

Aidha amekutwa na hatia, ikiwemo ya kumuingilia mtoto chini ya miaka 16, na hatia zingine nne za kuwafanyia vitendo visivyo vya kawaida watoto wa chini ya miaka 16.

Kiongozi huyu wa kanisa aliyekua anashikilia nafasi ya muweka hazina, na ni miongoni mwa viongozi wenye nguvu zaidi kanisani, anatarijiwa kuhukumiwa siku ya Jumatano huku mawakili wake wakisema kua watakata rufaa hatia hiyo.

Kwa mujibu wa shirika la utangazaji la Uingereza BBC, limeripoti kwamba Pell alikua katika mwaka wa kwanza katika kanisa huko Melbourne mwaka 1996 alipowafanyia unyanyasaji watoto , baada ya kuwaambia kuwa “walikunywa mvinyo wa kanisa” hivyo aliwalazimisha kufanya vitendo visivyofaa kama adhabu yao.

Kanisa lilipata fursa ya kusikia ushahidi kutoka kwa mmoja wa wahanga wa unyayasaji huo, huku muathiriwa mwingine akiwa ameshafariki.

Kadinali Pell amekanusha kuhusika na matukio yote , na kwa sasa yupo katika mapumziko wakati wote wa kesi hii ikiendelea.


Like it? Share with your friends!

0