JWTZ yasema vijana walioshiriki kujenga ukuta wa Mererani, wataajiriwa wote


0

Mkuu wa Majeshi nchini Jenerali Venance Mabeyo, amesema kutokana na mchakato wa ajira zao kuchukua muda mrefu, vijana waliokosa ajira walikuwa wakiwasiliana na viongozi mbalimbali ili kujua hatma yao, hali iliyowafanya kuhisi kwamba ahadi ya ajira isingetekelezeka.

 

“Vijana hao wanatakiwa waripoti wakiwa na nyaraka zao ikiwemo cheti walichotunukiwa baaa ya kukamilisha ule mradi wa Mirerani

Pili aje na mkataba wa kumaliza mafunzo ya JKT kwa wale ambao tayari wameshamaliza mkataba “

Katika mkutano na wanahabari leo, Jenerali Mabeyo, amesema azma ya ajira ipo kwa vijana hao ambao bado wapo kwenye kambi za Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), na amewataka wanapomaliza mikataba yao wakaripoti katika kambi ya JKT Mgulani kuanzia Septemba 12 mwaka huu, ili kuhakikiwa na kukamilisha taratibu za kuajiriwa jeshini.

Jenerali Mabeyo, amesema pia iko dhana miongoni mwa vijana wanaojiunga JKT, kwamba hatima yake watapata ajira kwenye majeshi ya ulinzi na usalama hasa wanapomaliza mkataba wao na kwamba dhana hiyo siyo sahihi

Takribani vijana 2033 waliopatiwa mafunzo kupitia Operesheni Kikwete na Operesheni Magufuli wanalengwa katika utekelezaji wa ahadi hiyo


Like it? Share with your friends!

0