Junker amwambia Johnson makubaliano ya Brexit hayawezi kubadilishwa


0

Rais wa halmashauri ya Umoja wa Ulaya Jean-Claude Junker, amemwambia waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson, kwamba maafisa wa Umoja wa Ulaya hawana idhini ya kufanya mashauriano mapya kuhusu makubaliano ya Uingereza kujitoa katika umoja huo, wa Brexit.

Junker na Boris Johnson walizungumza kwa njia ya simu kwa mara ya kwanza tangu Johnson alipoapishwa kuwa waziri mkuu.

Boris Johnson anatarajiwa kuiongoza Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya ifikapo Oktoba 31, iwe kwa makubaliano au bila makubaliano.

Baada ya mazungumzo yao ya simu, ofisi ya Junker imesema mkuu huyo wa halmashauri ya Umoja wa Ulaya alisisitiza msimamo wa Umoja wa Ulaya kwamba makubaliano yaliyoafikiwa ndiyo bora na ndiyo makubaliano pekee yanayowezekana kulingana na muongozo wa Umoja wa Ulaya.


Like it? Share with your friends!

0