Jinsi ajali ilivyokatisha uhai wa Edward Sokoine


1
1 point

Ni miaka 35 sasa imepita tangu aliyekuwa WazirI Mkuu wa zamani Hayati Edward Moringe Sokoine afariki dunia kwa ajali ya gari.

Hayati Sokoine alizaliwa mnamo tarehe 1/8/1938 katika wilaya ya MAASAI LAND, ambayo kwa sasa inafahamika kama wilaya ya Monduli, wilaya iliyoko mkoani Arusha.

Hayati Sokoine alipata elimu yake ya msingi Monduli, akafaulu na kujiunga na shule ya sekondari Umbwe, hii ilikuwa ni kuanzia mwaka 1948 mpaka 1958. Alipomaliza hapo alijiunga rasmi na chama cha TANU 1961, kisha alipata nafasi ya kwenda nchini Ujerumani mwaka 1962 mpaka 1963, kusomea mambo ya uongozi na utawala, na aliporudi akateuliwa kuwa Afisa Mtendaji wilaya ya Maasai Land.

Kutokana na ufanyaji kazi wake uliotukuka wilayani Monduli, wananchi hawakuwa na budi kumchagua kuwa mwakilishi wao bungeni yaani mbunge wa Monduli, na ufanisi wake kiutendaji ulionekana machoni mwa watendaji wakuu wa Serikali na hata kwa hayati baba wa taifa Mwl Nyerere. Kutokana na ufanisi wake huo akafanikiwa kuchaguliwa  kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mawasiliano na Usafiri hii ilikuwa mwaka 1967.

Hayati baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere akiwa na hayati Edward Sokoine

Kama hiyo haitoshi nyota ya kiuongozi huyo ilizidi kumwangazia ambapo mwaka 1972 aliteuliwa kuwa Waziri wa Usalama, na hatimaye mwaka 1977 aliteuliwa rasmi kuwa Waziri Mkuu wa iliyokuwa Serikali ya Tanganyika na Muungano wa Tanzania.

Hayati sokoine alikuwa hasa mzalendo na aliependa siasa za ujamaa na hata kupelekea kumwomba baba wa taifa ruhusa ya kusisimama kwa mda kama Waziri Mkuu, ili aende kusomea zaidi mambo ya ujamaa nchi za nje, hii ilikuwa mwaka 1981.

Mwaka 1983, alirudi kuendelea kama Waziri Mkuu wa Tanzania mpaka siku ya tarehe 12/4/1984, alipopata ajali mbaya ya kugongwa na gari lililotajwa kuwa  lilikuwa likiendeshwa na mkimbizi wa kisiasa, kutoka nchini Afrika kusini aliyejulikana zaidi kwa jina la Dube, eneo la Wami Dakawa ambayo kwa sasa inafahamika kama Wami Sokoine mkoani Mororgoro.

Pichani ni gari alilopatanalo ajali Hayati Edward Moringe Sokoine

Ajali iliyopelekea mauti yake palepale, kifo ambacho mpaka leo kinaacha maswali mengi, na kwa bahati mbaya hakuna hata mwandishi mmoja aliefanya mahojiano na bwana Dube ambaye kwa sasa yupo nchini Afrika kusini.

MCHANGO WAKE KWA TAIFA NA MISIMAMO NA MITAZAMO YAKE

1:Aliamini katika Haki,Usawa na uwajibikaji
2:Aliamini katika siasa za ujamaa zaidi ya siasa yeyote ile.
3:Aliamini kwamba maendeleo huja kwa watu kujituma kufanya kazi halali na bidii.
4:Aliamini katika mabadiliko chanya
5:Alikuwa mzalendo hasa kwa taifa hili
6:Aliichukia vitendo vya rushwa,hujuma,uhujumu uchumi,ulanguzi na magendo.
7:Alikuwa mtu wa vitendo na kamwe alikuwa si mtu wa kupenda kulalamikalalamika.

MCHANGO WAKE KITAIFA

1:Alikuwa mstari wa mbele enzi za vita ya Kagera pindi tunampiga Nduli Idd Amini.
2:Alianzisha vita dhidi ya uhujumu uchumi,biashara ya Ulanguzi,Magendo na aliichukia Rushwa kwa vitendo
3:Alikuwa mzalendo wa kweli wa taifa hili.
4:Aliamni katika siasa na kilimo,akiamini kilimo ni uti wa mgongo wa taifa hii ilipelekea kutotaka kupanda ndege ili ashuhudie juhudi kubwa za Watanganyika katika suala la kilimo
5:Alitunza na kutukuza tamaduni za kiafrika na utaifa wa mtanzania

Hakika Edward Moringe Sokoine ni Mzalendo na Shujaa wa taifa hili, hata hivyo yanayofanyika sasa katika siasa hususani katika Serikali ya awamu ya tano yalianza kuonekana tangu katika uongozi wa Sokoine kwani ameondoka yeye lakini nukuu zake zimebaki kama chachu ya kuwakumbusha viongozi wanapaswa kufanya nini.

“Ole wao wale wanaotumia nafasi zao za umma na serikali, kuiba, kuhujumu uchumi, kupokea rushwa, maana salama yao ni kudra za Mwenyezi Mungu labda nisiwajue” –Hayati Edward Moringe Sokoine, Waziri Mkuu wa zamani

Haya ni maneno yake ambayo hadi sasa yanaishi, na aliyazungumza wakati akihutubia kwenye mkutano kikao cha NEC mjini Dodoma.

 

 


Like it? Share with your friends!

1
1 point