Jeshi la Polisi latoa mafunzo kwa Askari


0

Arusha, Tanzania

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro amesema kuwa, askari Polisi wa Jeshi hilo wamepata mafunzo ya kutosha yatakayowawezesha kukabiliana na matishio mbalimbali ikiwemo uhalifu na mbinu nyingine za kuwashughulika wanaovunja sheria.
Amewataka Makamanda wa Polisi wa Wilaya kutoa elimu kwa askari wao ili wasiwe chanzo cha matatizo wakati wa uchaguzi.
IGP Sirro mesema hayo leo akiwa jijini Arusha, wakati akizungumza na maofisa wa Jeshi hilo ambapo amewasisitiza kuendelea kutoa elimu kwa wananchi Katika mikutano ya ulinzi shirikishi wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu.
“watoe elimu ya wapiga kura, wazungumzie sheria na kanuni zinazotawala uchaguzi ili kusaidia wakati mwingine watu wetu wanafanya makosa kwasababu ya kutokujua sheria kanuni” alisma IGP Sirro

IGP Sirro amewahakikishia wananchi kuwa, uchaguzi utakwenda vizuri kama ulivyopangwa na wale wachache wanaotegemea kufanya fujo hawatapata nafasi hiyo na kwamba Jeshi la Polisi litaendelea kutenda haki na watakaokiuka watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.


Like it? Share with your friends!

0