Iran yafuta mazungumzo na Trump


0

Rais wa Iran, Hassan Rouhani, ameondoa uwezekano wa kufanya mazungumzo na Rais Donald Trump, licha ya juhudi za dakika za mwisho za viongozi wa mataifa ya Ulaya wanaotaka kupunguza mvutano  huo, wakati  Marekani ikiongeza tena vikwazo vya adhabu dhidi ya Iran.

Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron kwa siku mbili bila ya mafanikio amekuwa akijaribu kuwakutanisha viongozi hao wawili wakiwa katika Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Macron anajaribu kufanikisha mkutano huo wa kihistoria ambao anatumai utaepusha kutokea vita katika Mashariki ya Kati.

Lakini Rouhani, akihutubia katika hadhara kuu ya Umoja wa Mataifa, amesema hatokubali kufanya mazungumzo wakati Marekani inaendelea kuiwekea vikwazo nchi yake.

 


Like it? Share with your friends!

0