Ifahamu Ijumaa Kuu


0

 

Ijumaa Kuu ni siku ambayo wa Kristo ulimwenguni kote wanaungana kuadhimisha mateso na Kifo cha bwana wao YESU Kristo msalabani. Aliyeletwa kuukomboa ulimwengu uliyojaa dhambi.

Kufuatana na taarifa za injili nne zilizoko ndani ya Biblia yaani Injili ya Mathayo, Marko, Luka na Yohana zinaeleza kuwa Yesu alisulubiwa siku moja kabla ya sabato yaani ijumaa. Mahali pakumsulubishia palikuwa ni katika mlima GOLIGOTHA nje ya kuta za mji wa Yerusalemu.

Siku hii haina tarehe thabiti katika kalenda ya kawaida ila tu hutangulia kabla ya Pasaka, hii hutokana na mabadiliko ya tarehe za Pasaka.

Licha ya mapokeo kuwa tofauti kati ukristo wa magharibi na ule wa mashariki, Ijumaa kuu inafuatana na adhimisho la Yesu kuingia mji wa Yerusalemu huku akishangiliwa sana kama mfalme wa Wayahudi, adhimisho hilo linafanyika mwanzoni mwa wiki na hujulikana kama jumapili ya matawi.

Wakristo duniani wanakumbuka mateso na kifo cha bwana wao Yesu Kristo katika siku kama ya leo yaani ijumaa kuu  kisha kulala kaburini siku ya jumamosi na kufufuka kwakwe siku ya jumapili.

 


Like it? Share with your friends!

0