Uncategorized

Human rights watch waigeukia Sudan


0

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu yaani Human Rights Watch, limewataka wafadhili na washirika wa kigeni nchini Sudan, waishinikize nchi hiyo izingatie haki, sheria na mabadiliko kwenye taasisi wakati serikali inapoendelea kutatua matatizo yake ya kiuchumi
Wito huo umetolewa leo, wakati ikitarajiwa kufanyika kwa mkutano ulioandaliwa na marafiki wa Sudan, utakaofanyika mjini Berlin nchini Ujerumani kwa ajili ya kuisaidia nchi hiyo kiuchumi.
Mkurugenzi wa shirika hilo kwa ukanda wa Afrika Mashariki, Jehanne Henry, amewataka viongozi wa Sudan na wale wa taasisi za kimataifa kuutumia mkutano huo kupanga jinsi nchi hiyo itakavyosonga mbele, ili mabadiliko ya uongozi yaliyofanyika yafanikishe njia sahihi hasa kwenye masuala ya uongozi na haki za binadamu.

 


Like it? Share with your friends!

0