Gwajima aikataa video ya utupu


0

Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, amekana kuhusika kwenye video ya faragha inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikimuhusisha yeye ambapoa amesema kuwa video hiyo imetengenezwa.

Gwajima amesema hayo  leo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo amenukuliwa akisema “Hiyo video aliyeisambaza ni mtu mmoja anajiita The Originaleast wa mtandao wa Instagram, na sijui ameitengeneza hivyo akiwa na maana gani na siku zote ukikuta mtu amerusha tukio la mtu au watu wakiwa chumbani jua nia yake si nzuri”. Amesema Gwajima

Ameongeza kuwa  “Naomba mjiulize ni mwanamume gani anaweza kujirekodi mwenyewe halafu ajiwekee mikono ya baunsa alafu aitume kwenye mitandao? lengo la mtu huyu haliwezi kuwa zuri na ana lengo la kunichafua,” amesema Gwajima.

Aidha, Gwajima amesema tayari amesharipoti Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kuhusu video hiyo na ameripoti Polisi na kupewa RB.

 


Like it? Share with your friends!

0