Gadiel atua Simba!


0

Klabu ya Simba imemtambulisha beki, Gadiel Michael, baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili na mabingwa hao.

Usajili wa Gadiel umemaliza tetesi za muda mrefu kuwa anajiunga na Simba akitokea Yanga akiwa mchezaji huru kama ilivyokuwa kwa mshambuliaji Ibrahimu Ajibu.

Mbali ya Simba kumtambulisha Gadiel pia jina lake tayari lilikuwa katika orodha ya wachezaji wao iliyopelekwa CAF tayari kwa mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Akizungumzia usajili wake, Gadiel alisema atapambana ili kupata namba kwenye kikosi cha kwanza cha Mabingwa hao wa Ligi Kuu.

Gadiel anacheza beki namba mbili nafasi anayocheza Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ alisema nguzo pekee itakayompa namba kwenye kikosi cha kwanza ni kujituma na kujiamini huku akitolea mfano wakati anatoka Azam FC kwenda Yanga aliamini katika kujituma.


Like it? Share with your friends!

0