Farasi watumika kutengeneza dawa ya COVID 19 Argentina


0

Wanasayansi nchini Argentina wametengenza dawa kutoka katika kinga ya mwili wa farasi ambayo imeonesha uwezo wa kuzuia maambukizi ya virusi vya corona

Dawa hiyo ambayo ni sehemu ya majimaji katika seli za damu za farasi tayari imeonesha kufifisha virusi katika maabara na itaanza kufanyiwa majaribio kwa binadamu kuanzia mwezi ujao

Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, Wanasayansi wanasema dawa hiyo ina kinga ya mwili ambayo inauwezo wa kufanya virusi visiongezeke na kuzia kabisa kuingia mwilini.

Matumizi ya dawa hiyo pia inaruhusu mgonjwa kujijengea kinga binafsi ya mwili ya kuzuia magonjwa

Wanasayansi hao wanasema Farasi ana uwezo mkubwa wa kuleta majibu kwa haraka, kwani baada ya kufanyiwa jaribio ya kinga hiyo walileta majibu ndani ya wiki moja badala ya mwezi .

Anasema kuwa katika kipindi cha juma moja wameweza kutoa kiasi cha lita 20 ya sehemu ya majimaji katika seli za damu za farasi

Dawa hiyo ni mahususi kwa ajili ya kuwapa wagonjwa katika hatua za mwanzo za kuumwa


Like it? Share with your friends!

0